IQNA- Usomaji wa Qur'ani Tukufu kwa hakika unaweza kutajwa kuwa 'Sauti ya Mbinguni', ambao kila aya zake tukufu huleta thawabu kubwa na usikilizwaji wake huleta utulivu wa mioyo. Katika mfululizo wa "Sauti ya Mbinguni", tumekusanya nyakati za hamasa, unyenyekevu, na uzuri wa sauti ya Qur'ani, na sehemu bora za tilawa ya wasomaji mashuhuri wa Kiirani, ili kuwa urithi wa kusikika wa fani ya tilawa na maana ya kiroho ya aya za Qur'ani.
Ifuatayo ni sehemu ya tilawa ya Ustadh Younes Shahmoradi, msomaji wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu nchini Iran. Tunatumai kuwa kazi hii itakuwa hatua ndogo kuelekea kufahamu na kujikurubisha zaidi na maneno ya Wahyi.
Tilawa hii ni sehemu ya aya ya 286 ya Suratul Baqarah: