IQNA

Hafidh wa Qur’ani kutoka Hamedan kuwakilisha Iran Mashindano ya Bangladesh

15:17 - December 16, 2025
Habari ID: 3481666
IQNA – Mehdi Barandeh, mmoja wa wawakilishi wa Iran katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur’ani nchini Bangladesh, anatarajiwa kuondoka kuelekea nchi hiyo ya Asia Kusini mwishoni mwa wiki hii.

Barandeh, mzaliwa wa mji wa Hamedan uliopo magharibi mwa Iran, aliieleza IQNA kuwa atashiriki katika Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Bangladesh katika kitengo cha uhifadhi wa Qur’ani Tukufu.

Amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa na makundi mawili: tilawa na hifdhi.

Kwa mujibu wake, Bangladesh ilituma mialiko kwa wizara za mambo ya nje za nchi mbalimbali, na baada ya tathmini kufanyika, wale wanaokidhi vigezo vya kiufundi na umri ndio huchaguliwa kushiriki katika tukio hilo la Qur’ani.

Akaongeza: “Hapa Iran, mimi na Bwana Is’haq Abdullahi tulikidhi masharti hayo, na tukateuliwa kuiwakilisha nchi katika tilawa na hifdhi, mtawalia.”

Akizungumzia ushiriki wake wa awali katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, Barandeh alisema aliwahi kushinda nafasi ya kwanza katika hifdhi ya Qur’ani nzima kwenye Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Saudi Arabia.

Kwa upande mwingine, Abdollahi, qari kutoka Iran, alishika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya 23 ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Urusi.

Toleo la nne la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Bangladesh linatarajiwa kufanyika jijini Dhaka kuanzia Desemba 19 hadi 24.

/3495746

captcha