Taarifa hiyo ilitoa wito kwa Idara ya Mahakama kuhakikisha kuwa wahusika wa vurugu na vitendo vya kigaidi wanapelekwa mbele ya sheria kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu. Aidha, ililaani kitendo cha kuvunjwa heshima ya misikiti, kuchomwa kwa nakala za Qur’ani, pamoja na kuuliwa kwa watu wasio na hatia na walinzi wa usalama mikononi mwa wahalifu hao.
Jumuiya hiyo ilisisitiza kuwa wale waliokuwa na silaha na kuua raia pamoja na maafisa wa usalama wanapaswa kupewa adhabu kali zaidi. Ikielekeza lawama kwa kile ilichokiita ushiriki wa Marekani “mhalifu” na utawala wa Israel “muovu” katika kuchochea vitendo hivyo, taarifa hiyo ilikumbusha kuwa Jamhuri ya Kiislamu imepitia fitina nyingi katika historia yake na mara zote imetoka kifua mbele.
Katika siku za Alhamisi na Ijumaa, wahalifu wenye vurugu waliharibu mali za umma na binafsi katika miji kadhaa nchini Iran, na kusababisha vifo vya raia na maafisa wa usalama, huku wengine wakijeruhiwa. Wahalifu hao walivunja miundombinu ya umma, wakazuia barabara, wakashambulia majengo ya serikali na vituo vya polisi, na kuwajeruhi maafisa wa usalama na vyombo vya sheria waliokuwa wakijaribu kurejesha utulivu.
3496043