IQNA

Jeshi la IRGC liko tayari kuvunja njama za Marekani na Israel dhidi ya Iran

14:22 - January 15, 2026
Habari ID: 3481805
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amezionya Marekani, Israel na mamluki wao wenye mienendo ya kigaidi kama ile ya Daesh kwamba kosa lolote la kimahesabu litakabiliwa na majibu makali na ya kuangamiza.

Katika taarifa yake, Meja Jenerali Mohammad Pakpour amesema IRGC bado iko kwenye kiwango cha juu cha utayarifu wa kusambaratisha 'njama za udanganyifu' zilizobuniwa na Ikulu ya White House na Tel Aviv.

Jenerali Pakpour amewataja wale waliohusika na machafuko ya hivi karibuni nchini kuwa ni "mamluki wenye mtindo wa Daesh" wanaofanya kazi chini ya uongozi wa mataifa ya kigeni.

"IRGC yenye nguvu na inayoungwa mkkono na wananchi iko katika kiwango cha juu cha utayarifu wa kutoa jibu kali kwa mahesabu mabovu ya adui na mamluki wao wa ndani wenye mienendo ya Daesh," amesema Jenerali Pakpour.

Amesema: "Kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu, na kupitia umoja mtakatifu wa taifa la Iran, tutabatilisha mipango ya watawala wa Ikulu ya White House na Tel Aviv dhidi ya Iran Imara."Jeshi la IRGC liko tayari kuvunja njama za Marekani na Israel dhidi ya Iran

Kamanda wa IRGC amemtaja Rais wa Marekani, Donald Trump, na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kama wasanifu wakuu wa umwagaji damu wa hivi karibuni nchini Iran.

Meja Jenerali Mohammad Pakpour amemtaja Trump kuwa ni "mcheza kamari mhalifu" na "Nimrod wa wakati huu," na Netanyahu kuwa ni "muuaji wa watoto," akisema "uhalifu wao wa kikatili" kote nchini Iran hautasahaulika kamwe na utakabiliwa na kulipizwa kisasi wakati unaofaa.

Habari inayohusiana

Jenerali Pakpour pia amepongeza maandamano makubwa ya kitaifa yaliyofanyika Januari 12 kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu na kupinga njama za maadui, akisifu "ufahamu na ujasiri" wa Wairani waliosimama kwa mshikamano na mashahidi wa usalama.

Amesema idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika shughuli ya mazishi ya mashahidi wa mashambulizi ya kigadi ya hivi karibuni hapa nchini imeonyesha heshima isiyoyumba ya taifa na kupinga mashinikizo ya kigeni na ugaidi unaofadhiliwa na serikali za Marekani na Israel.

3496069

captcha