Muhammad Issa amesema kuwa hadi sasa nchi 43 zimetangaza kwamba zitatuma wawakilishi katika mashindano ya 11 ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur’ani. Ameongeza kuwa filamu ya matukio ya kweli (documentary) ya historia ya mashindano hayo ya kimataifa inatayarishwa.
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Algeria amesema washindi wa mashindano hayo wataemziwa na kutunzwa katika sherehe kubwa itakayofanyika katika Msikiti Mkuu wa Algiers.
Mashindano ya 11 ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Algeria yamepangwa kufanyika tarehe 20 hadi 26 za mwezi mtukufu wa Ramadhani na yatasimamiwa na Rais Abdul Aziz Bouteflika wa nchi hiyo.