Akizungumza Jumapili usiku mjini Beirut kwa mnasaba wa kuanza mwezi wa Muharram na kukumbuka masaibu ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake watiifu katika ardhi ya Karbala, Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea matukio mbalimbali katika nyanja za kisiasa, kiusalama, kifikra, kidini, kiuchumi kiimani na kijamii na kusisitiza kwamba, leo hii umma wa Kiislamu unapaswa kuwa macho katika kukabiliana na changamoto kubwa ya makundi ya kitakfiri na kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na hasa katika nchi za Lebanon, Iraq na Syria.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kuna udharura mkubwa wa kutumiwa vyema siku hizi za maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi huu wa Muharram na kuwataka viongozi wa Lebanon kuwa makini katika kuzima njama zilizopangwa za kuzusha fitina na mifarakano kaskazini mwa nchi hiyo.
Sayyid Nasrullah amelielezea tukio la Karbala na kusisitiza kwamba, tukio hilo litaendelea kubaki katika historia ya mwanadamu kwani limepelekea kuhifadhiwa Uislamu na watu wote wanajukumu la kubainisha kilichojiri katika ardhi ya Karbala…/mh