IQNA-Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali mauaji ya kiongozi maarufu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Sheikh Rasoul Shahoud, aliyeuawa katika shambulizi lililotokea katika mkoa wa Homs, Syria ya kati.
Habari ID: 3480939 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/13
IQNA – Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, amekataa wazo la kusalimisha au kuachana na silaha za harakati hiyo ya mapambano, akisema kuwa wanaotaka hilo wanapaswa kwanza kulaani na kutaka mwisho wa uvamizi wa Israeli dhidi ya Lebanon.
Habari ID: 3480902 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/05
IQNA-Sheikh Naim Qassem, kiongozi wa harakati ya muqawama ya Lebanon Hizbullah ameeleza kuwa Israel si tu kuwa inaikalia kwa mabavu Palestina bali ni tishio la kimkakati kwa Lebanon, Misri, Syria, Jordan, na ni tishio pia kwa amani na usalama wa kanda hii na dunia nzima kwa ujumla.
Habari ID: 3480888 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/03
IQNA-Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem amezungumzia shambulio la hivi karibuni la utawala wa Kizayuni kwenye viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut, na akasema: "shambulio hili limefanywa kwa idhini na uungaji mkono wa Marekani."
Habari ID: 3480608 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/29
IQNA – Katibu Mkuu wa Hizbullay ya Lebanon amepuuzilia mbali wazo la kuipokonya harakati hiyo, silaha zake na kusema wale wanaotoa wito wa kufanya hivyo wanahudumia ajenda ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Habari ID: 3480562 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/19
IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Lebanon, Hizbullah, imetoa wito kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL), vituo vya kielimu na kisayansi vya Umma wa Kiislamu, pamoja na wapenda uhuru duniani kuchukua hatua za haraka kutimiza wajibu wao wa kihistoria kuhusu Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480554 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/17
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qassim, amesema katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuwaenzi makamanda waliouawa shahidi kwamba: Haj Imad Mughniyah alikuwa shakhsia wa kiusalama na kijeshi na mbunifu ambaye aliwaongoza Mujahidina kwa msingi wa moyo wa imani.
Habari ID: 3480230 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/17
IQNA – Hizbullah imepanga kufanya mazishi ya Katibu Mkuu wake , Hizbullah Sayed Hassan Nasrullah, pamoja na Mkuu wa Baraza lake la Utendaji, Shahidi Hashem Safiyyuddin, Februari 23, 2025.
Habari ID: 3480151 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/03
Muqawam
IQNA - Israel ililazimika kuomba kusitisha mapigano kutokana na uwezo wa Hizbullah, amesema katibu mkuu wa harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon.
Habari ID: 3480008 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/05
Muqawama
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa Marekani na washirika wake wanakoseka kikamilifu wanapodhani kwamba Muqawama umeishiwa nguvu na umefika ukingoni.
Habari ID: 3479913 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/17
Muqawama
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria ushindi wa harakati ya muqawama katika kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel, na kutaja kuwa kusimama kidete na kujitolea muhanga wapiganaji wake kama sababu kuu zinazopelekea ushindi huo.
Habari ID: 3479902 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/15
Shahidi
IQNA - Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza mahala alipozikwa Sayed Hashem Safieddine, mkuu wa Halmashauri Kuu ya harakati hiyo ambaye aliuawa shahidi mwezi Oktoba.
Habari ID: 3479875 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/08
IQNA - Maelfu ya watu wa Lebanon wanarejea makwao kusini mwa Lebanon baada ya kusitishwa kwa mapigano kati ya utawala haramu wa Israel na Harakati Hizbullah. Mapatano hayo yalivikiwa Jumatano iliyopita.
Habari ID: 3479836 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/02
Muqawama
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, wanamapambano wa kambi ya Muqawama wako tayari kuendelea kupambana na adui wakati wowote watakapolazimika kufanya hivyo.
Habari ID: 3479825 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/30
Muqawama
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameipongeza Lebanon na harakati yake ya Muqawama, Hizbullah kwa kufanikiwa kusimamisha vita vya Israel, na kuutaja kuwa ni "ushindi wa kimkakati kwa Hizbullah na wa kufedhehesha" kwa utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3479822 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/28
Muqawama
IQNA - Harakati ya muqawama ya Lebanon Hizbullah imesema imepata ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni, na kuongeza kuwa adui Mzayuni alijidanganya na hivyo alishindwa kudhoofisha azma ya Hizbullah.
Habari ID: 3479821 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/28
Muqawama
IQNA - Tarehe itatangazwa hivi karibuni kwa ajili ya mazishi ya marehemu kiongozi wa Hizbullah Shahidi Sayed Hassan Nasrallah, mbunge wa Lebanon alisema.
Habari ID: 3479816 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/27
Muqawama (Mapambano ya Kiislamu)
IQNA- Hatimaye baada ya miezi 14 ya vita vikali kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, usitishaji vita wa siku 60 umeanza kutekelezwa asubuhi ya leo (Jumatano) baina ya pande hizo mbili.
Habari ID: 3479815 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/27
Muqawama
IQNA-Kiongozi wa Hizbullah amesema harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon iko tayari kupigana vita vya muda mrefu dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, na kwamba jibu lao kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya anga dhidi ya Beirut litakuwa kulenga katikati mwa Tel Aviv.
Habari ID: 3479786 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/21
Jinai za Israel
IQNA - Harakati ya Muqawama ya Lebanon, Hizbullah, imetoa rambirambi kwa kuuawa shahidi Mohammad Afif al-Nablusi katika shambulio la Israel lililolenga jengo moja katikati mwa Beirut.
Habari ID: 3479769 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/18