Akihutubia waombolezaji wa Abaa Abdillah Imam Hussein AS katika mkesha wa Ashuraa kusini mwa Beirut, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, machafuko na mapigano yanayoshuhudiwa katika nchi za Libya, Syria, Iraq na Lebanon ni ya kisiasa na wala hayafungamani na misingi ya itikadi za Kishia wala Kisuni, lakini kwamba madola ya kibeberu ya Magharibu yanajaribu kuzifungamanisha hitilafu hizo na masuala ya kimadhehebu na kikabila, ili yaweze kuwatumia wafuasi wa madhehebu moja dhidi ya wafuasi wengine, kwa ajili ya kufikia malengo yao haramu. Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kwamba silaha za Hizbullah ziko dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi ya kitakfiri na kiwahabi, ambayo yana azma ya kuuangamiza ulimwengu wote. Katibu Mkuu wa Hizbullah amewataka wafuasi wa madhehebu ya Kisuni na Wakristo nchini Lebanon kuwa macho na matukio yanayojiri katika eneo. Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kwamba siku ya Ashuraa ni siku ya hamasa, siku ya kuulinda Uislamu na siku ya kuhuishwa na kufungamana na malengo aali ya Imam Hussein AS...mh