IQNA

Maonyesho ya kaligrafia ya aya za Quran katika ukumbi wa Kamal al Molk

12:09 - November 09, 2008
Habari ID: 1706135
Maonyesho ya kaligrafia (sanaa ya kuandika vizuri) ya aya za Quran chini ya anuani ya "Hati Katika Patineh" yanayojumuisha kazi za Mohammad Bani Ahmad na wanafunzi wake yemefunguliwa Jumamosi Novemba 8 katika ukumbi wa Kama al Molk mjini Tehran.
Akizungumza na waandishi habari kuhusu hati ya "Patineh", Bani Ahmadi amesema kuwa, "Hati katika Patineh" ni athari za kaligrafia zinazoandika juu ya ngozi".
Ameongeza kuwa, "athari nyingi za Quran zimeandikwa kwa hati kama vile Nastalikh, Shekaste na grafiki".
Kaligrafia ya Quran ni sanaa ya kale katika ulimwengu wa Kiislamu iliyoenea kutoka Indonesia hadi Senegal. Sanaa hii inahesabiwa kama mojawapo wa sanaa muhimu katika ustaarabu adhimu wa Kiislamu. 317211
captcha