IQNA

Turathi za Kiislamu

Vioo vya Msikiti wa Rangi ya Waridi nchini Iran kukarabatiwa

21:05 - September 08, 2024
Habari ID: 3479398
IQNA Vioo vya rangi katika Msikiti wa Nasir-ul-Mulk - pia unaojulikana kama Msikiti wa Rangi ya Waridi - vinakarabatiwa, kulingana na afisa wa mkoa.

"Ukarabati wa madirisha ya msikiti umekamilika, na ukarabati wa vioo kwa sasa unaendelea," alisema Mohammad Reza Esfandi, msimamizi wa maeneo ya kihistoria yanayoendeshwa na Shirika la Wakfu la Mkoa wa Fars.

“Tumeagiza vioo hivyo kwa vile ni vya aina maalum na tunakusudia kubadilisha vioo vilivyovunjika na kuchakaa,” aliongeza.

Msikiti wa Nasir-ul-Molk ni msikiti wa zama za Qajar huko Shiraz kati mwa Iran. Msikiti unajumuisha vioo vingi vya rangi na pia una vitu vingine vya kitamaduni.

Mwangaza wa jua unapoangaza kupitia vioo hivyo vya rangi, huleta uzuri wa aina yake  na kufanya msikiti huu upendeze sana. “Mbinu iliyotumika katika msikiti huu ni kwamba hakuna kemikali iliyotumika katika ukarabati wa milango na madirisha,” alisema na kuongeza kuwa kazi zote za milango ya mbao ya msikiti huo zilifanywa kwa kutumia maliasili na bidhaa.

Kipaumbele kikubwa katika ukarabatiwa  wa msikiti huu kilikuwa ukarabati wa paa, kwani unyevu ulikuwa umepenya ndani ya jengo kutokana na mvua, Esfandi alibainisha na kuongeza kuwa paa la pande zote mbili za msikiti kwa sasa linarejeshwa. 

4235418

captcha