IQNA

Chuo cha Kiislamu cha Madina kuanzisha kanali ya satalaiti

9:12 - November 13, 2008
Habari ID: 1707722
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha mji mtakatifu wa Madina kitaanzisha kanali ya televisheni ya Satalaiti hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia, Muhammad bin Ali al-Uqalaaa amesema kuwa lengo la televisheni hiyo ni kupambana na ugaidi, misimamo ya kupindukia mipaka, kuondoa fikra potofu na kusambaza ulimwenguni ujumbe wa Uislamu ambao ni wa fikra na mitazamo ya wastani kitika kila jambo. Amesema kuwa televisheni hiyo itakuwa ikionyesha na kutangaza moja kwa moja ratiba na vipindi vinavyofundisha katika Chuo Kikuu cha Madina na kuongeza kuwa hiyo itakuwa ni hatua muhimu katika kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahadhiri na wanachuo kupitia teknolojia ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi moja kwa moja kutoka mbali. Chuo cha Kiislamu cha Madina kilibuniwa mika saba iliyopita na hadi sasa kimeandaa mikutano na warsha mbalimbali za kupambana na ugaidi na kuwasilisha mitazamo ya wastani ambapo wasomi na wanafikra mbalimbali wa Kiislamu wameshiriki na kutoa michango yao. Chuo hicho vilevile mwaka ujao kinapanga kuandaa kikao kingine cha kimataifa katika uwanja huohuo. 319334
captcha