IQNA

Yemen yatangaza kupiga marufuku ya meli za Israel kupita Bahari ya Sham

17:38 - June 08, 2026
Habari ID: 3482337
IQNA-Vikosi vya Jeshi la Yemen vimetangaza marufuku kamili ya usafiri wa baharini wa Israel katika Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham), vikisema kwamba harakati zote za adui katika eneo hilo sasa zitachukuliwa kuwa malengo halali ya kijeshi, baada ya kutekeleza shambulizi la kombora lenye usahihi dhidi ya maeneo nyeti ya Israel huko Tel Aviv.

Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu, likiwa sehemu ya makabiliano mapana ya Yemen ya kukabiliana na “uchokozi wa Marekani na Wazayuni” dhidi ya mhimili wa muqawama unaojumuisha Iran, Palestina, Lebanon, Iraq na Yemen.

Msemaji wa jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree, amesema mashambulizi ya makombora yalilenga eneo la Yaffa linalokaliwa kwa mabavu ambalo limepachikwa jina la Tel Aviv.  Amesema operesheni hiyo imetekelezwa kwa mafanikio na usahihi mkubwa.

Kwa mujibu wa Jenerali Saree, operesheni hiyo ilitekelezwa kupinga mradi wa Kizayuni unaolenga kuanzisha kile kinachoitwa “Israel Kubwa” chini ya nadhari ya eti “Mashariki ya Kati Mpya.”

Aidha amesema operesheni hiyo inalenga kuvunja “mzingiro dhalimu uliowekwa na adui wa Kimarekani” dhidi ya watu wa Yemen pamoja na mataifa ya mhimili wa muqawama nchini Lebanon, Gaza na Iran.

Jenerali Saree amesema operesheni hiyo ilitekelezwa kwa kuzingatia kanuni ya umoja wa medani za mapambano katika kukabiliana na maadui, na pia kama jibu la moja kwa moja kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, Iran na Gaza.

Ameendelea kusema kuwa: “Jaribio lolote la adui litashindwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na operesheni zetu zitaendelea mradi uchokozi na mzingiro dhidi yetu na dhidi ya mhimili wa jihadi na muqawama utaendelea,” alisema msemaji huyo.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kujitolea kwa Yemen kudumisha umoja wa medani za mapambano pamoja na Iran, Hizbullah nchini Lebanon, na makundi ya muqawama katika Palestina na Iraq, katika kukabiliana na kile wanachokitaja kuwa mradi wa Kizayuni na utawala wa Marekani katika eneo hilo.

Awali, Israel ilitangaza Jumatatu asubuhi kwamba kombora lilikuwa limerushwa kutoka Yemen kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.

3497760

captcha