Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Ma'a hekalu hilo litafunguliwa mwezi Disemba. Hekalu hilo limejengwa pembizoni mwa Msikiti wa Al Aqsa na ujenzi wake unahesabiwa kuwa ni tishio kubwa kwa jengo la Msikiti wa Al Aqsa. Khalil Tofcachi ameongeza kuwa kuba la hekalu hilo limejengwa kiwango sawa na msikiti wa Qubbat al-Swakhra na kwa hivyo kuwa kuzuizi kwa msikiti huo. Ameongeza kuwa: Ufunguzi wa hekalu hilo kubwa zaidi la Kiyahudi duniani utapelekea kuharibika athari za kihistoria na Kiislamu katika mji wa Quds na kulifanya hekalu hilo lizingatiwa zaidi".
Khalil Tofcachi amedokeza kuwa, Utawala wa Kizayuni unatekeleza mpango wa kuupa mji wa Quds utambulisho kamili wa Kiyahudi ifikapo mwaka 2020 na kuhakikisha kuwa wakaazi Waarabu katika mji wa Quds hawatazidi asilimia 12.
Msomi huyo wa Palestina amesema kuwa iwapo nchi za Kiarabu na Kiislamu zitaendelea kunyamazia kimya hatua hizo za kinyama na zisizo za kibinadamu za Israel, hatima ya Quds itakuwa sawa na Andalusia. 319532