IQNA

Taarifa ya mwisho ya Duru ya Pili ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu

14:49 - November 15, 2008
Habari ID: 1708420
Mashindano ya Kimataifa ya Qura’ani Tukufu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu yalimalizika jana mjini Tehran kwa kutolewa taarifa ya mwisho.
Taarifa hiyo ambayo ilisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Majaji wa mashindano hayo imesisitiza juu ya umuhimu wa kushimakana na Qur'ani Tukufu kama kitabu cha uongofu na ufanisi wa mwandamu. Taarifa hiyo imesema: Qurani Tukufu ni ufunuo wa Mwenyezi Mungu usiokuwa na mbadala, kanuni ya uongofu na kitabu cha saada na ufanisi wa mwanadamu mbacho mafunzo na miongozi yake inaweza kuiokoa dunia ya leo iliyojaa machafuko kutoka kwenye masaibu na matatizo mengi ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni ma kuwadhaminia saada wanadamu. Taarifa hiyo imesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikihubiri umoja kati ya Waislamu kwa kuzingatia Qur'ani Tukufu na kufuatia mazingatia maalumu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Iran kwa vijana na wanafunzi wa vuo vikuu, Tehran inalizingatia suala la kueneza maarifa ya Qur'ani katika vyuo vikuu kuwa ni hatua ya thamani na yenye taathira kubwa katika njia ya kufikia malengo aali ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. Imesema: Ni kwa msingi huo ndiyo maana taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu na Jumuiya ya Shughuli za Qur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini inaiona hatua yoyote katika uwanja huo kuwa ni taufiki ya Mola Muumba.
Jumuiya hizo zimeitisha mashindano ya mwaka huu ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi 40 duniani baada ya mafanikio ya duru ya kwanza ya mashindano hayo.
Kiwango na ubora wa mashindano ya mwaka huu ambayo yalisimamiwa na maustadhi na shakhsia wakubwa wa fani ya kusoma Qur'ani kama Ustadh Abul Einein Sheisha na majaji wengine kutoka Misri, Ufilipino, Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mahudhurio makubwa ya vijana wa Qur'ani wa umma wa Kiislamu ni bishara ya mashindano makubwa na bora zaidi ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafanya juhudi zote kuhakikisha kwamba yanaendelea kufanyika.
Taarifa ya mwisho ya Kamati ya Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu imewashuruku watu na jumuiya zote zilizochangia katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu. Imesisitiza kwamba kusoma, kuhifadhi na mashindano ya Qur'ani Tukufu ni utangulizi wa kukifahamu kwa undani kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kufanyia kazi mafundisho yake.
320046
captcha