IQNA

Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Lyon kushiriki katika kugawa zawadi kwa wahitaji

10:53 - November 18, 2008
Habari ID: 1709564
Katika kipindi hiki cha kukaribia sikukuu ya Idilhaj, Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa mji wa Lyon, Ufaransa umetangaza kwamba uko tayari kushiriki katika shughuli za taasisi ya Richard ya kugawa zawadi kati ya watoto wagonjwa na wasiokuwa na makazi wa taasisi hiyo
IQNA imenukuu kituo cha habari cha Islamcrunch kwamba lengo la kutekeleza mpango huo ni kuwaliwaza na kuwafariji watoto hao wagonjwa au wasiokuwa na makazi ambao wanahitaji msaada wa makundi mbalimbali. Kwa sababu hiyo Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Lyon umewataka Waislamu wote wa Ufaransa kukabidhi zawadi na misaada yao ya kifedha kwa viongozi wa msikiti huo ili ziwasilishwe kwa watoto wagonjwa wa kituo cha Richard wakati wa Idilhaji.
Shughuli zote za utekelezaji wa mpango huo wa kibindamu za kukusanya na kugawa zawadi kwa watoto wagojwa wa kituo ch Richard zitapigwa picha na kuchapishwa katika mtandao rasmi wa intaneti wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Lyon. 321672
captcha