Mkutano wa kuarifisha sira na suna za Mtume Muhammad SAW hususan kwa watu waliosilimu karibuni na wasiokuwa Waarabu umeanza mjini Madina, Saudi Arabia ukisimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu.
Wazungumzaji wa kwanza wa mkutano huo walijadili sira na suna za Nabii Muhammad kwa lugha za Urdu, Bangla, Amhari, Burmese, Kiindonesia, Kiingereza na Kifilipino.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu mjini Madina Mustafa bin Ali Alawi amesema kuwa lengo la kuitishwa mkutano huo ni kuyaelewesha mataifa ya dunia sira na suna za Mtume Muhammad SAW na sifa njema za kimaadili za Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu. Ameongeza kwamba kandokando ya mkutano huo kutakuwepo harakati na shughuli mbalimbali za kiutamaduni. Amesema kutafanyika pia maonyesho ya vitabu vilivyotafsiriwa kwa lugha mbalimbali na maonyesho ya picha ya jamii za waliowachache huko Saudi Arabia. 322741