Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Saudi Arabia, warsha hiyo inasimamiwa na Abdulah bin Abdul Muhsin at-Turki, Katibu Mkuu wa jumuiya iliyotajwa na lengo lake kuu ni kuchunguza njia za kuarifisha misingi na mafundisho ya dini hii tukufu katika nchi zisizokuwa za Kiislamu. Vilevile njia za kuimarisha mazungumzo ya nchi za Kiislamu na nchi nyinginezo kwa lengo la kuuarifisha Uislamu ulimwenguni ni maudhui nyingine inayopewa uzito katika warsha hiyo. Warsha hiyo imefanyika mjini Makka pambizoni mwa kikao cha tisa cha kimataifa cha 'kuujua Uislamu katika nchi zisizo za Kiislamu, ukweli na mustakbali.'
Uchunguzi wa maendeleo yaliyofikiwa katika kuuarifisha Uislamu kwa wasio Waislamu, changamoto na vikwazo vilivyopo katika njia ya kuenezwa Uislamu katika nchi zisizokuwa za Kiislamu na Mustakbali wa uhubiri wa Kiislamu ni miongoni mwa maudhui ziliozopewa uzito katika warsha hiyo ya siku tatu mjini Makka. 328896