IQNA

Kikao cha kila mwaka cha Taasisi ya Twawaf ya Mahujaji wa Ulaya mjini Makka

10:23 - December 03, 2008
Habari ID: 1715377
Kikao cha kila mwaka cha Taasisi ya Twawafu ya Mahujaji wa Nchi za Ulaya kimefanyika mjini Makka kuchunguza ibada ya kupiga mawe nembo ya shetani wakati wa ibada ya Hija.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wanachama wa Taasisi ya Twawafu ya Mahujaji wa wa Ulaya, viongozi wa Wizara ya Hija ya Saudi Arabia, wakuu wa misafara ya Hija ya nchi mbalimbali na taasisi zinazosimamia ibada ya Hija.
Wail bin Saleh Halabi, afisa wa idara inayosimamia amali ya kupiga mawe nembo ya shetani amesema kuwa kikao hicho cha kila mwaka kimechunguza namna ya kuwaelimisha mahujaji jinsi ya kutekeleza ibada hiyo na taratibu zitakazotumiwa na makundi mbalimbali ya mahujaji wakati wa kutekeleza amali hiyo ya Hija.
Amesema, malengo mengine ya kikao hicho ni kuboresha huduma kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, kujenga mawasiliano ya mara kwa mara kati ya ujumbe mbalimbali za Hija na viongozi wa serikali ya Saudi Arabia na kudhamini usalama na amani kwa mahujaji. 328870

captcha