IQNA

Mafunzo ya misingi ya Uislamu maalumu kwa wanawake wa Ghana

12:53 - December 04, 2008
Habari ID: 1715794
Duru ya kujifunza misingi na thamani za dini ya Uislamu maalumu kwa wanawake wa Kiislamu wa Ghana, imeanza katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la ar-Riyadh, Mafunzo hayo ambayo yataendelea kwa muda wa wiki moja yamedhaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Uhubiri wa Kiislamu na yanafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Asim kilichoko katika mji mkuu. Mkuu wa jumuiya hiyo mjini Accra amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, mafunzo hayo yatatolewa na walimu wa jumuiya hiyo na kwamba yatajumuisha ibada katika Uislamu, nafasi ya mwanamke katika Uislamu na nafasi ya mama wa Kiislamu katika kulea kizazi kijacho. 329338
captcha