IQNA

Salamu za pongezi za Idul Adh'ha za Rais wa Syria kwa Waislamu

9:31 - December 08, 2008
Habari ID: 1717011
Rais Bashar al- Asad wa Syria amewatumia ujumbe wa pongezi na fanaka Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idul Adh'ha.
Shirika Rasmi la Habari la Syria Sana limeripoti kuwa, Rais Asad amewatumia ujumbe wa pongezi viongozi wote wa nchi za Kiislamu akiwatakia fanaka na kheri kwa mnasaba huu mtukufu. Wakati huohuo, Mufti Mkuu wa Syria, Waziri wa Sheria, Waziri wa Wakfu na Kadhi Mkuu wa nchi hiyo pia wamemtumia rais huyo jumbe tofauti za kumpongeza na kumtakia maisha marefu kwa mnasaba huu muhimu kwa nchi za Kiislamu. 330944
captcha