Mtandao wa intaneti wa ‘mathaba.net’ umeandika kwamba, mtoto mkubwa wa kiume wa Kanali Muammar Gaddafi, Seiful Islam Gaddafi ameteuliwa kusimamia mchakato wa kutazama upya katiba ya nchi hiyo akishirikiana na wataalamu kutoka nchi za Ulaya na Marekani.
Qur’ani Tukufu imekuwa msingi wa katiba ya Libya tangu mwaka 1977 ambayo pia inategemea vipengee vya kitabu cha Green Book kilichoandikwa na Kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
Uamuzi wa viongozi wa Libya wa kutoitambua Qur’ani kama chanzo kikuu cha sheria za katiba ya nchi hiyo umechukuliwa katika hali ambayo wananchi wote wa nchi hiyo ni Waislamu. 334359