IQNA

Jumuiya za kimataifa, waungaji mkono wakubwa wa utawala wa Kizayuni

17:28 - December 24, 2008
Habari ID: 1722559
Mkurugenzi wa gazeti la al Wifaq linalochapishwa mjini Tehran amesema kuwa sababu ya kwanza ya kukubalika jumuiya yoyote ya kimataifa na kuruhusiwa kubakia katika medani ni kuunga mkono sera za kisiasa na kiuchumi za nchi za Magharibi na kutoufanyia uhasama utawala ghasibu wa Israel.
Musib al Nuaimi ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya nchi za Kiarabu, amesema kuwa jumuiya za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na mashirika yake, Benki ya Dunia na taasisi zenye mfungamano na jumuiya hizo za kimataifa ambazo zina makao Marekani, Geneva au katika nchi nyingine za Ulaya, zinadhibitiwa kikamilifu na madola makubwa kama Marekani.
Ameashiria mgogoro wa Palestina mbao ni changamoto kubwa ya jamii ya kimataifa na akasema: Mgogoro huo hauwezi kutatuliwa kwa kutegemea utendaji wa jumuiya za sasa za kimataifa na kwamba ni mapambano ya wananchi wa Palestina pekee ndiyo yatakayoleta ufumbuzi wa hali hiyo. al Nuaimi amesema kuwa taarifa zinazotolewa na nchi za Magharibi na jumuiya za kimataifa baadhi ya wakati kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina huwa na lengo la kuzihadaa fikra za waliowengi na kupotosha ukweli wa mambo.
Amelaani mzingiro wa Israel dhidi ya wakazi milioni moja na nusu wa Ukanda wa Gaza na akasema: Jinai hiyo inafanyika kwa uungaji mkono wa Marekani na nchi za Magharibi na haitakomeshwa isipokuwa kwa mapambano ya wananchi wa Palestina wenyewe na si kwa msaada wa jumuiya za kimataifa. 336761


captcha