IQNA

Katibu Mkuu wa OIC:

Mashambulio ya Israel huko Gaza ni jinai ya kivita

10:37 - December 29, 2008
Habari ID: 1724172
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) imelaani mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina na kutaja unyama huo wa Wazayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia kuwa ni jinai ya kivita.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu imesema: Jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya raia wasiokuwa na hatia wa Palestina ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na makubaliano ya Geneva ambayo yanasisitiza juu ya kulindwa raia wakati wa vita.
Katibu Mkuu wa OIC ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kusimamisha jinai hizo za Israel. Ihsanoglu amezitaka pia harakati na makundi ya Palestina kukomesha hitilafu zao na kuungana katika kukabiliana na adui wao. 339369
captcha