Vyuo hivyo vimetoa taarifa vikitangaza kwamba, kutokana na mauaji ya umati yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wanawake na watoto wasio na hatia wa Gaza, pamoja na hatua yake ya kulipua ovyo makazi ya raia, misikiti na vituo vya kielimu vya Gaza na hasa Chuo cha Kiislamu cha eneo hilo, wanachuo na wahadhiri wa vyuo hivyo kote nchini Iran wako tayari kutekeleza amri yoyote itakayotolewa na Kiongozi Muadhamu kuhusiana na jinai hizo za utawala wa Kizayuni.
Taarifa hiyo imesema kuwa, wanachuo na wafanyakazi wa vyuo hivyo vya Qur'an sambamba na Waislamu wa maeneo mengine ya dunia, wameshiriki kwa wingi katika maandamano makubwa ya kulaani jinai hizo ambazo zinatekelezwa na Wazayuni huku ulimwengu unaodai kuwa umestaarabika na kutetea haki za binadamu, ukiwa umeketi kimya bila kuchukua hatua yoyote ya maana katika kuzua mauaji yanayofanywa na utawala huo dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.
Taarifa hiyo pia imebainisha hasira na masikitiko makubwa kutokana na kimya na hata ushirikiano wa baadhi ya watawala wa Kiarabu na utawala wa Tel Aviv katika kuwakandamiza na kuwaua kwa umati Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. 340918