IQNA

Kituo cha Kimataifa cha Mazungumzo ya Dini Mbalimbali nchini Qatar chataka kusimamishwa mauaji huko Gaza

10:50 - January 01, 2009
Habari ID: 1725910
Kituo cha Kimataifa cha Mazungumzo ya Dini Mbalimbali cha Qatar kimelaani mauaji ya kinyama yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasiokuwa na hatia wa Ukanda wa Gaza na kutaka mauaji hayo yasimamishwe.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imezitaka jamii eti zilizostaarabika za Magharibi na zinazodai kutetea haki za binadamu kufanya juhudi za kusimamisha haraka mashambulizi ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo imesema kuwa jinai zinazofanywa na Israel ni ubaguzi wa kizazi na kuongeza kuwa, mashambulizi ya anga ya Israel yanakiuka mafundisho ya dini za mbinguni na sheria na kanuni za kimataifa na kwamba yanatishia amani na usalama wa dunia nzima.
Imeongeza kuwa jinai zinazofanywa na Israel katika eneo la Gaza zitaharibu juhudi za kurejesha amani, maelewano na kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini na tamaduni tofauti.
Taarifa hiyo imemalizia kwa kusisitiza kwamba, inasikitisha kuona kuwa viongozi wa nchi za Kiarabu wameamua kunyamaza kimya na kupuuza vilio vya watoto wadogo na wanawake wasiokuwa na hatia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na pia vilio vya majeruhi wa jinai za utawala wa Kizayuni. 341667
captcha