IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'ubunifu katika fikra za Kiislamu' nchini Yemen

11:12 - January 03, 2009
Habari ID: 1726382
Kikao cha kimataifa cha 'ubunifu katika fikra za Kiislamu; udharura, malengo na vidhibiti' kimepangwa kufanyika mjini Sanaa, mji mkuu wa Yemen tarehe 16 Februari.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Watan kikao hicho kitaandaliwa na Muungano wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu na kwa ushirikiano wa Vyuo Vikuu vya Sanaa na Iman.
Khalid Tamim, Mkuu wa Chuo cha Sanaa amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, Wahadhiri 40 kutoka vyuo mbalimbali vya Kiislamu watahudhuria kikao hicho ambapo watazungumzia umuhimu wa kuainishwa malengo na ubunifu katika fikra za Kiislamu. Amesema mbali na suala hilo, washiriki pia watajadili na kuchunguza masuala mbalimbali ya fiqhi ya Kiislamu na vilevile mambo mengine yanayowahusu wanazuoni na wasomi wa Kiislamu. 342416
captcha