Jumuiya hiyo inayozishirikisha taasisi 15 muhimu za Kiislamu nchini humo imelaani vikali mashambulio hayo yanayofanywa na utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu na kusema kuwa, mashambulio hayo ni mauaji ya kizazi dhidi ya Waislamu.
Taarifa ya jumuiya hiyo imezitaka jumuiya za kutetea haki za binadamu ulimwenguni kufanya juhudi za kusimamisha mauaji hayo ya umati dhidi ya raia wasio na ulinzi na kuulani utawala haramu wa Israel kuhusiana na mauaji hayo. Taarifa hiyo imewataka Waislamu wote ulimwenguni kusimama na kuwateta wenzao wanaokabiliwa na jinai pamoja na mauaji ya umati huko Gaza. Imesema kuwa, huo sio wajibu wa kisheria tu bali ni wajibu wa kibinadamu na kimaadili pia kwa Waislamu wote. Imesema, Waislamu wanapasa kuwa kitu kimoja na kusimama imara mbele ya dhulma na uonevu unaofanywa dhidi ya Waislamu wenzao. Imesema, hii inatokana na hadithi ya Mtume Mtukufu (saw) kuwa Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwenzake na kwamba Muislamu hapasi kupuuza na kumwacha ndugu yake Muislamu ateseke. 342415