Gazeti la Misri la al-Akhbar limesema kuwa idadi hiyo ya wahubiri na wasomi wa Kiislamu wametoa taarifa hiyo wakitaka umma wa Kiislamu kuunga mkono na kutetea Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas dhidi ya jinai zinazotekelezwa dhidi yake na Wazayuni. Taarifa hiyo imewataka Waislamu kutekeleza majukumu yao ya kidini na kisheria kwa kuwaunga mkono kwa hali na mali wananchi wa Palestina wanaodhulumiwa na kukandamizwa kinyama na utawala ghasibu wa Israel. Taarifa hiyo pia imezitaka nchi za Kiarabu kukata mara moja uhusiano wao wa kisiasa na utawala huo haramu pamona na nchi nyingine zinazouunga mkono utawala huo. Wanazuoni hao wa Kiislamu wamesema kuwa mashambulio ya kinyama yanayoendeshwa na utawala haramu wa Israeol huko katika Ukanda wa Gaza yanakiuka thamani zote za kibinadamu na kimaadili na kutaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kufanya jitihada za kumaliza hujuma hiyo ya kinyama ya Wazayuni dhidi ya watu wasio na hatia. Taarifa hiyo imewataja Wazayuni kuwa kundi la wavamizi na wachokozi ambao wanapaswa kutofautishwa na Mayahudi. Imemtaka kila Muislamu kufanya juhudi za kuikomboa Gaza kutoka kwenye makucha ya wavamizi wa Kizayuni na utawala ghasibu wa Israel. 344208