IQNA

Aljeria, mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Ustahamilivu Katika Uislamu

12:06 - January 10, 2009
Habari ID: 1728824
Kongamano la kimataifa la Ustahamilivu Katika Uislamu linatazamiwa kufanyika mwezi ujao wa Februari nchini Aljeria. Kongamano hilo litasimamiwa na Baraza Kuu la kiislamu la nchi hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Aljeria Abu Imran al Sheikh amesema kuwa kongamano hilo litahidhuriwa na wanazuoni wa Kiislamu, wanafikra, wahadhiri wa vyuo vikuu vya Kiislamu na vya Ulaya. Ameongesza kuwa watafiti na wataalamu wa masuala ya mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali kutoka mabara ya America na Asia pia watahudhuria kongamano hilo la kimataifa.
Sheikh Abu Imran al Sheikh amesema kuwa miongoni mwa malengo ya kongamano hilo ni kueneza thamani kamavile ustahamilivu na juhudi za kuzuia fikra za kuchupa mipaka zinazopingwa na mafundisho ya dini ya mbinguni. 345283
captcha