IQNA

Israel haitaheshumu azimio la Baraza la Usalama

9:52 - January 11, 2009
Habari ID: 1729095
Israel haitaheshimu azimio la Baraza la Usalama la kuitaka kusimamisha vita huko Gaza licha ya kuwa baraza hilo ndio taasisi kubwa zaidi ya kudhamini usalama na amani duniani.
Gazeti la Ar Riyadh la Saudi Arabia limemnukulu Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu anayeshughulikia masuala ya Palestina na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu Muhammad Sabih akiyasema hayo na kuongeza kuwa: "Israel haijafikia malengo yake katika hujuma yake huko Ghaza na badala yake imepata hasara kubwa".
Ameashiria hotuba za Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel Ehud Olmert na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala huo Tzipi Livni waliosema kuwa hawataheshimu azimio la Baraza la Usalama na kuongeza kuwa azimio hilo lina nukta chanya ambayo ni sisitizo lake la usitishwaji vita.
Afisa huyo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ametaka kufanyike juhudi za kuwaunganisha Wapalestina na nchi za Kiarabu ili kufanikisha utekelezwaji azimio hilo. Aidha amesema, kunahitajika misaada ya kuyajenga upya maeneo ya Wapalestina yaliyoharibiwa kwa mashambulizi ya Israel.
Amesema, pamoja na kuwepo upinzani wa Marekani, lakini jitihada za nchi za Kiarabu zilifanikisha upasishwaji azimio la Baraza la Usalama lilioutaka utawala wa Kizayuni kusitisha vita mara moja huko Gaza. 345750
captcha