IQNA

Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari yalaani kuharibiwa ofisi za televisheni za Iran huko Gaza

13:49 - January 12, 2009
Habari ID: 1729664
Jumuiya ya Kimatafa ya Waandishi Habari, IUJ, imetoa taarifa ikilaani hatua ya wanajeshi wa Kizayuni wa Israel ya kuhujumu kwa makombora ofisi za televisheni za Kiirani za Al Alam na Press TV katika Ukanda wa Gaza.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waandishi Habari Aidan White ametoa taarifa mjini Brussels Ubelgiji na mbali ya kulaani kitendo hicho cha Wazayuni amewataka waandishi habari kujitokeza na kuandamana kupinga mashinikizo ya utawala wa Kizayuni dhidi ya vyombo vya habari yanayolenga kuficha ukweli kuhusu matukio ya Gaza.
Taarifa hiyo ya IUJ imesema kuwa: “Hivi sasa waandishi wa habari wanapata matatizo makubwa kuingia Gaza kufanya mahojiano na wahanga wa jinai za Israel mbali na kuwa hadi sasa waandishi habari kadhaa wameuawa baada ya kushambuliwa na jeshi la Israel”.
Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Januari vifaru vya utawala wa Kizayuni, katika kitendo kinachokiuka sheria za kimataifa za kinga ya wanahabari, vilishambulia ofisi za kanali za televisheni za Al Alam na Press TV mjini Gaza na kuepelekea mwandishi habari moja kujeruhiwa na vile vile kuharibi jengo hilo.
Hatua hiyo ya jeshi la utawala haramu wa Israel inatokana na hasira ya Wazayuni kufuatia habari sahihi zinazotangazwa na kanali hizo mbili kuhusu jinai za Israel huko Gaza. 346258
captcha