IQNA

Kongamano la tatu la Uchumi wa Kiislamu kufanyika leo Malaysia

13:43 - January 12, 2009
Habari ID: 1729959
Kongamano la tatu la Uchumi wa Kiislamu limeanza leo katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Shirika la habari la Malaysia Bernama limeripoti kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili njia za kuimarisha uchumi katika jamii za Kiislamu.
Malengo mengine ya kongamano hilo ni kuzidisha uwezo wa nchi za Kiislamu katika nyanja za uwekezaji, utumiaji wa matokeo ya utafiti mbalimbali na kustafidi na fursa za kiuchumi.
Kongamano hilo la siku nne ambalo linasimamiwa na Jumuiya ya Ustawi wa Kiuchumi wa Kiislamu ya Malaysia na Baraza la Kiislamu la nchi hiyo limefunguliwa kwa hotuba ya Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Tun Razzaq. 346531
captcha