IQNA

Wasomaji Qur'ani wa kike wa Kuwait wakusanyika kuiunga mkono Gaza

10:41 - January 13, 2009
Habari ID: 1730314
Wasomaji na mahafidhi wa Qur'ani wa kike wa Kuwait wamekutana katika kituo cha Qur'ani cha Abdulatif al Umar kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wanaokandamizwa wa Ukanda wa Gaza.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limeripoti kuwa, Nayif al Ajami, mhadhiri wa teolojia ya Kiislamu wa Kuwait alihutubia mkutano huo akisema kuwa matukio ya Gaza yamedhihirisha unyama wa Israel katika kuamiliana na raia wasiokuwa na hatia wa Palestina na njama za utawala huo za kutekeleza mauaji ya kizazi katika Ukanda wa Gaza.
Nayif al Ajami ameongeza kuwa, katika mashambulizi hayo ya kinyama Israel inauwa kwa umati watu wote bila ya kutofautishi baina ya askari, mtoto, mwanamke na wazee.
al Ajami amesema, wakazi wa Gaza wanahitaji msaada wa ndugu zao Waarabu na Waislamu na kwamba ni wadhifa wa kidini na kibinadamu kuwasaidia raia wa Gaza.
Wasomaji Qir'ani wa kike walioshiriki kwenye mkutano huo walionyeshwa picha ya jinai zinazoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na wakakusanya misaada mbalimbali iliyotolewa kwa ajili ya wakazi wanaodhulumika wa eneo hilo. 346366

captcha