Kiongozi wa kundi la Jama't Islamiya la Pakistan amesema kuwa upuuzaji wa jumuiya za kimataifa na baadhi ya Waislamu kuhusu mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya raia wasiokuwa na hatia wa Palestina, unatia aibu.
Qadhi Hussein Ahmad ameyasema hayo katika maandamano makubwa ya kupinga jinai za Israel yaliyofanyika mjini Islamabad.
Amesema kuwa makundi ya Kiislamu yanapaswa kuwaunganisha Waislamu na kuanzisha harakati za kuwaokoa wakazi wa Gaza.
Qadhi Ahmad amesema kuwa, mapigano ya jihadi ndiyo njia pekee ya kupambana na dhulma za Wazayuni. Ameashiria kuwa maelfu ya wanajihadi wako tayari kwenda Gaza kuwasaidia Wapalestina na akasisitiza kuwa badala ya kuandamana na kutoa nara tupu, Waislamu wanapaswa kuchukua maamuzi ya kivitendo na kufanya jitihada za kuyatekeleza.
Kiongozi wa Jama't Islamiya nchini Pakistan ameitaka Misri kufungua kituo cha mpakani cha Rafah kwa ajili ya kuingiza misaada ya dawa na chakula kwa wakazi wa Gaza badala ya kufanya juhudi za kuiridhisha Marekani kwa kufunga kituo hicho. 347105