IQNA

Madaktari wa Norway: Matukio ya Gaza ni sawa na maafa ya Sabra na Shatila

11:57 - January 14, 2009
Habari ID: 1730700
Madaktari wawili wa Norway wamesema baada ya kurejea nchini kwao kutoka Gaza walikochunguza hali ya mambo ya eneo hilo kuwa, hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na hatia na kuwaua kinyama inashabihiana na mauaji ya umati yaliyotekelezwa pia na Wazayuni huko Sabra na Shatila mwaka 1982.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Islamonline, madaktari hao wawili wa Norway Mads Gilbert and Erik Fosse ambao pia walikuwepo wakati wa mauaji ya kinyama yaliyotekelezwa na Wazayuni huko Sabr na Shatila nchini Lebanon wamelaani vikali jinai za sasa za Israel huko Gaza na kutangaza kuwa: “ Hujuma hii inapaswa kusimamishwa haraka iwezekanavyo na mipaka ifunguliwe ili wakazi wasio na hatia wa Gaza wapelekewe maji, chakula na suhula za kitiba”.
Madaktari hao wawili wamesisitiza kuwa, kinyume na madai ya Israel, asilimia 90 ya majeruhi wanaotibiwa katika mahospitali ya Gaza ni raia.
Mbali na kutekeleza mauaji ya umati huko Gaza, utawala wa Kizayuni pia umeharibi nyumba za raia, mashule, mahospitali na misikiti. Aidha utawala katili wa Israel umekuwa ukitumia silaha za sumu dhidi ya raia wa Gaza.
Tangu kuanza hujuma ya utawala dhalimu wa Israel huko Gaza, karibu Wapalestina 1000 wasio na hatia wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya 4000 wakijeruhiwa vibaya. Asiliami 90ya wahanga ni raia wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Itakumbukwa kuwa mauaji ya Sabra na Shatila yalijiri kati ya tarehe 16-18 Septemba mwaka 1982 wakati Wazayuni na vibaraka wao wa kundi la wanamgambo wa Kikristo wa Kifalanja wa Lebanon wakiongozwa na katili Ariel Sharon waliposhambulia kambi ya wakimbizi wa Palestina kusini mwa Lebanon na kuwaua kwa umati Wapalestina kati ya 700-3500. Hujuma hiyo ilifanyika kulipiza kisasai cha mauaji ya Rais Bashir Gemayel wa Lebanon kutoka kundi la Wakristo Wamaronite.
Wafalanga ni kundi la Wakristo wenye misimamo mikali nchini Lebanon ambao waliunga mkono kikamilifu uvamizi wa Israel nchini humo na walihusika na vitendo vya mauaji ya umati ya Wapalestina kusini mwa Lebanon. 347641
captcha