IQNA

Kamati ya uhakiki wa kimataifa ichunguze jinai za Israel huko Gaza

9:33 - January 20, 2009
Habari ID: 1733301
Jumuiya ya Madaktari wa Kiarabu imetoa taarifa mwishoni mwa kikao chake huko Cairo Misri ikitaka kubuniwa kamati ya kimataifa ya kuhakiki jinai za kinyama zilizotekelezwa na utawala haramu wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha siku 22 za uchokozi wake dhidi ya watu wasio na hatia katika ukanda huo.
Taarifa hiyo imesema kuwa wengi kati ya watu waliouawa katika Ukanda huo ni wanawake na watoto na kwamba jambo hilo linabainisha wazi kiwango cha jinai zilizotekelezwa na Wazayuni katika Ukanda huo. Imesisitiza kuwa jinai hizo zinabainisha wazi utambulisho wa mauaji wa utawala huo na kutoheshimu kwake sheria za kimataifa.
Taarifa hiyo imeashiria kuuawa kwa baadhi ya madaktari katika mashambulio hayo ya Israel huko Gaza na pia hatua ya utawala huo ya kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa katika kuwaua kwa umati watu wasio na hatia na kutaka kuhukumiwa kwa watawala wa utawala huo haramu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Hiyo si mara ya kwanza kwa Isrel kutumia silaha zilizopigwa marufuku dhidi ya raia bali ulizitumia mwaka 2006 dhidi ya raia katika mashambulio yake ya kichokozi huko Lebanon. Mwishoni taarifa hiyo imekosoa vikali udhaifu wa taasisi za kimataifa katika kuzuia jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia na kuzitaka nchi za Kiislamu ziweke jinai hizo katika ratiba za masomo katika shule zao ili wanafunzi na kizazi cha baadaye kipate kutambua jinai na mauaji yaliyotekelezwa na utawala hou dhidi ya watu wasio na hatia. 350987
captcha