IQNA

Sisitizo la Ayatullah Hakim juu ya umuhimu wa kuhuishwa minasaba ya Kishia ulimwenguni

11:05 - January 25, 2009
Habari ID: 1735367
Ayatullah Sayyid Muhammad Said Hakim, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini Iraq amesisitiza juu ya umuhimu wa kuhuishwa nara za Imam Hussein (as) na minasaba ya Kishia ulimwenguni.
Shirika la Habari la As’wat al-Iraq limemnukuu Ayatullah Said Hakim alipokutana jana Jumamosi na kundi moja la wahuishaji wa maombolezo ya Imam Hussein (as) la Iraq huko katika mji mtakatifu wa Najaf kuwa, uhuishwaji wa maombolezo hayo pamoja na minasaba ya Kishia unapelekea kulindwa kwa itikadi na mafundisho ya Kiislamu katika kukabiliana na fikra potofu duniani.
Amesema, kuhuishwa kwa nara za Imam (as) kunazima njama za maadui wa Uislamu na makundi ya Kiwahabi za kutaka kufuta ukweli wa kihistoria na marasimu ya kidini ya Mashia. Ameongeza kuwa, kuharibiwa kwa makaburi ya maimamu watoharifu (as) katika makuburi ya Baqii pamoja na ya wake wa Mtume (saw) pamoja na mwanawe Ibrahim kulikofanywa na makundi ya Kiwahabi yenye misimmao ya kupindukia mipaka, ni ishara ya wazi inayothibitisha kwamba Mawahabi sio maadui wa Mashia tu bali wamelenga utamaduni mzima wa Uislamu. Ameendelea kusema kuwa, hatua ya baadhi ya waandishi ya kupotosha historia ya tukio la Ashura, waandishi ambao wanaungwa mkono kifedha na makundi ya Kiwahabi, inatokana na upotofu wao wa kuchanganya haki na batili kwa malengo yao binafsi.
Ayatullah hakim amewataka wahuishaji wa minasaba ya maombolezo kuzingatia takwa na kushikamana na masuala ya wajibu pamoja na thamani na vilevile mafundisho halisi ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). 353301
captcha