Mkuu wa chuo hicho amesema, anajifaharisha kuona kwamba chuo hicho kimefungua kitengo cha kuchunguza masuala ya dini mbalimbali na kwamba suala hilo litawasaidia wanafunzi na jamii ya Marekani kuzielewa vyema tamaduni mbalimbali. Amesema, kitengo hicho kitazidisha maarifa ya umma kuhusu utafiti wa masuala ya Kiislamu.
Amesema kuwa kuanzishwa kitengo cha utafiti wa dini makhsusi hakuna maana ya kufundisha dini hiyo kama inavyofanyika katika shule za kidini, na kwamba wanafunzi watakaohitimu masomo katika kitengo hicho watakuwa wataalamu wa masuala ya Kiislamu.
Chuo Kikuu cha North Carolina kiliasisiwa mwaka 1789 na kilikuwa chuo kikuu cha kwanza ambacho wanafunzi wake walihitimu masomo katika karne ya 18.
Kitengo cha Utafiti wa Masuala ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha North Carolina kinakusudia kutoa majibu kwa wanafunzi wanaotaka kuufahamu vyema Uislamu. 823663