Bunge la Uingereza limepitisha muswada uliowasilishwa na wabunge 50 wa bunge hilo kwa madhumuni ya kutangazwa matangazo ya misaada kwa ajili ya wahanga wa Palestina walioathirika kutokana na jinai za kivita za utawala haramu wa Israel, katika kanali zote za redio na televisheni za Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC.
Muswada huo ulipitishwa kwa wingi wa kura za wabunge 130. Wabunge hao wamewataka wakuu wa shirika BBC kufutilia mbali amri yao ya kuzuia kutangazwa katika kanali zote za shirika hilo, matangazo ya jumuiya za masuala ya kheri za nchi hiyo kwa ajili ya kukusanya misaada ya kibinadamu, vikiwemo vyakula na madawa, kwa ajili ya waathirika wa mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel.
Vilevile wabunge hao wamesema kuwa hatua ya waku wa BBC imetokana na satuwa pamoja na ushawishi wa lobi za Kizayuni katika shirika hilo na kupendelea kwake utawala wa Israel. Martin Linton, mbunge wa Uingereza kutoka chama cha Lebour amekosoa vikali msimamo wa wakuu wa BBC na kuwataka wabunge watoe mashinikizo zaidi kwa ajili ya kuwalazimisha kutangaza matangazo ya misaada kwa Wapalestina.
Wakati huohuo maelfu ya Waingereza wamefanya maandamano makubwa mbele ya jengo la BBC na kulaani vikali siasa za shirika hilo za kuupendelea utawala wa Israel na kutojali machungu ya watu wa Gaza. Idadi kubwa ya shakhsia wa kisiasa, kiutamaduni, kidini na wapinzani wa vita walishiriki katika maandamano hayo. 355629