IQNA

Mapambano, chaguo la kwanza la kujikomboa kutoka kwenye ubeberu

15:55 - February 03, 2009
Habari ID: 1737910
Katika siku za mwanzoni za mashambulio ya kinyama ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia wala ulinzi huko katika Ukanda wa Gaza, wataalamu wa mambo na watawala wa utawala huo ghasibu walikuwa wakidhani kwamba hatimaye Wapalestina wangesalimu amri mbele ya hujuma kali ya utawala huo na kuacha kupambana wala kutetea ardhi na utambulisho wao.
Lakini baada ya kuendekelea kwa mauaji ya umati ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusimama kidete na kisha kushinda kwa kishindo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, kumethibitisha wazi ukweli huu kwamba, mapambano daima ndilo chaguo la kwanza katika kujikomboa kutoka kwenye makucha ya madhalimu na madikteta wa zama hizi.
Kwa kuzingatia nguvu kubwa ya kijeshi ya utawala wa Israel na uungaji mkono mkubwa wa nchi za Magharibi na hasa Marekani kwa utawala huo, ni watu wachache sana waliodhani kwamba utawala huo hatimaye ungelazimika kutangaza usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza bila ya kufikia malengo yake uliyokuwa umeyatangaza mwanzoni mwa hujuma hiyo ya kinyama dhidi ya watu wasio na ulinzi. Licha ya suala hilo, lakini imani ya kimaanawi ya Hamas na kutegemea kwake uwezo wa Mwenyezi Mungu hatimaye kulipelekea harakati hiyo ya Kiislamu kushinda na kuudhalilisha utawala huo katika medani ya vita visivyo vya uwiyano wa kijeshi.
Kuhusiana na suala hilo, Hujjatul Islam wal Muslimeen, Muhammad Ridha Nur Ilahiyan, mtafiti wa masuala ya kidini anasema kuwa, kuuawa shahidi na kwa njia ya kidhulma viongozi wa Hamas akiwemo Sheikh Ahmad Yassin, kuliwapa moyo na nguvu kubwa za kimaanawi wanamapambano wa Hamas katika kukabiliana na hujuma kali ya utawala haramu wa Israel na hatimaye kuwafanya wawe washindi, licha ya utawala huo kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa dhidi ya watu wasio na hatia na hasa wanawake na watoto wa Ukanda wa Gaza.
Ali Asghar Iranmanesh, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Yemen pia amezungumzia suala hilo na kusema kuwa, wanapambano wa Hamas walipata ilhamu na mafunzo muhimu kutokana na mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala nchini Iraq, katika ushindi wao dhidi ya Wazayuni waliokuwa wamejizatiti vilivyo kwa silaha za kisasa kabisa.
Ali Ramadhan al-Ausi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha London ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha Masuala ya Kiarabu katika Kituo cha Kiislamu cha Uingereza anasema kuhusiana na jambo hilo kwamba, kumtegemea Mwenyezi Mungu kulikuwa na nafasi muhimu katika ushindi wa Hamas dhidi ya Wazayuni, na kuongeza kuwa, jambo hilo lilipelekea utawala wa Kizayni kukosea katika mahesabu yake yote ya kijeshi na kuwadhihirishia walimwengu udhaifu mkubwa wa mfumo wake wa habari za siri katika medani ya vita. 355381
captcha