IQNA

Kongamano la "Mapinduzi ya Kiislamu na Mapambano ya Gaza" kufanyika Iran

11:23 - February 05, 2009
Habari ID: 1740446
Kongamano la Mapinduzi ya Kiislamu na mapambano ya Gaza litafanyika tarehe 9 Februari kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika mji wa Qum kusini mwa Tehran, kongamano hilo litajadili mapambano ya fakhari ya wapigania ukombozi wa Palestina na namna walivyoathiriwa na Mapinduzi ya Kiisalmu nchini Iran.
Kongamano hilo litahutubiwa na Mkuu wa Idara ya Utamaduni na wanachuo wa kidini kutoka Pakistan, Hujattul Islam Raisi, na Imam wa Ijumaa wa mji wa Ahwaz kusini mwa Iran Hujjatul Islam Hujjati ambaye pia ni mkuu wa Chuo Kikuu cha Kidini cha Khuzestan.
Kongamano hilo litafanyika baada ya swala za Magharibi na Isha'a katika Chuo Kikuu cha Imam Khomeini MA. 359509
captcha