Kwa mujibu wa gazeti la al Sharq la Qatar, mkutano huo umesimamiwa na Kituo cha Utafiti wa Kieneo na Kimataifa cha Chuo Kikuu cha George Washington cha Marekani huko Qatar.
Sayyid Hussein Nasr alisema katika mkutano huo kwamba eneo la Ghuba ya Uajemi ni mojawapo na maeneo yenye utajiri mkubwa wa kimazingira duniani na kwamba nchi za kandokando ya eneo hilo zinawajibika kulinda eneo hilo la kistratijia.
Amesema kuwa moja kati ya hatari na changamoto kubwa zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu ni kwamba baadhi ya wasomi wa Kiislamu wanaamini kuwa ulimwengu wa Kiislamu unahitajia fikra na mitazamo ya Magharibi kwa ajili ya kujiondoa kwenye matatizo ya sasa.
Mwanafalsafa huyo wa Kiirani amesisitiza kuwa mabadiliko katika muundo wa mtazamo wa kifalsafa kuhusu mazingira yanahitaji utaalamu, jihudi za kifikra na ufahamu wa kina kuhusu turathi za Kiislamu na matumizi ya teknolojia na matunda ya kielimu ya Magharibi.
Hussein Nasr amemalizia kwa kusema kuwa nchi za Kiislamu zinaweza kutumia ada na maarifa ya Kiislamu katika kulinda mazingira yao. 360180