IQNA

Imam Khomeini (MA) alifungamanisha Mapinduzi ya Kiislamu na kadhia ya Palestina

18:07 - February 12, 2009
Habari ID: 1743191
Sheikh Mohammad Yazbek mwanachama wa Baraza la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa mwanzoni mwa kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA) alianzisha ukuraba na taifa la Palestina. Kwa kutuma misaada kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina, kiongozi huyo alisitiza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanashikamana vilivyo na kadhia ya Palestina.
Sheikh Muhammad Yazbek ameyasema hayo katika kikao cha wanafikra kilichofanyika mjini Beirut na kuongeza kuwa: "Leo Iran hini ya uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei imebakiwa kuwa ile ile Iran iliyokuwa chini ya uongozi wa Imam Khomeini (MA) na ingali inaunga mkono mapambano ya Palestina".
Sheikh Muhammad Yazbek mwanachama wa Baraza la Harakati ya Hizbullah ameashiria suala la baadhi ya watu kupinga mfumo wa Wilayatul Faqih au Utawala wa Faqihi na mwanazuoni wa kidini na kuwataja kuwa wanaofungamana na Marekani. Amesema, Utawala wa Faqihi ni utawala unaokwenda na sheria na kwamba hauna kifani duniani kwa mtazamo wa kimaadili, kiusalama na kielimu.
Mkutano huo wa wanafikra uliandaliwa na Idara ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon na kuhudhuria pia na Muhammad Hussein Raiszadeh Mwambata wa Utamaduni wa Iran, Imam wa Msikiti wa Quds wa mji wa Saidaa kusini mwa Lebanon Sheikh Mahir Hamud na mjumbe katika Bunge la Lebanon Marwan Faris.
Akizungumza pia katika kikao hicho Sheikh Mahir Hamud ameashiria baadhi ya watu wanaozusha hitilafu za kimadhehebu ili kufikia malengo yao haramu yakiwemo ya kuvuruga harakati ya mapambano ya Hizbullah ya Lebanon na kusema kuwa, watu kama hao wamefeli katika njama zao. Amesema Iran na Hizbullah, kinyume na madai ya baadhi ya nchi za Kiarabu, zimewasaidia watu wa Gaza pamoja na kuwa aghlabu yao ni wa madehehbu tafauti.
Naye Marwan Faris amesema matukio ya hivi karibuni katika Ukanda Gaza yanaonyesha kuwa matumaini ya mataifa huru duniani kuhusu kuangamizwa Israel yanaweza kufikiwa. 362131




captcha