Dakta Haddad Adel amesema kuwa mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yaliyaondoa mapambano ya kupigania uhuru ya Palestina katika mipaka ya utaifa na Uarabu na kuyapa sura ya Kiislamu.
Ameashiria matukio ya Palestina katika kipindi chote cha miaka 60 iliyopita na akasema: Katika karne ya 19 serikali ya Kiothmani iliyokuwa na makao makuu mjini Istanbul Uturuki ilitawala sehemu kubwa ya dunia ya Kiislamu na kulinda umoja wa nchi za Kiislamu. Amesema, nchi za Magharibi hususan Uingereza zilisambaratisha serikali hiyo na kuligawa eneo la Mashariki ya Kati katika vijisehemu vidogo vidogo. Spika wa zamani wa Bunge la Iran amesema kuwa hatua hiyo ilikuwa mwanzo wa janga kubwa zaidi ambalo ni kupandikizwa mti habithi wa Israel katika dunia ya Kiislamu na katika hatua iliyofuatia Uingereza iliasisi utawala huo haramu na kuufanya rasmi katika Umoja wa Mataifa.
Haddad Adel amesema kuwa wananchi wa Iran walikataa kuutambua rasmi utawala huo bandia tangu ulipoasisiwa na daima wamekuwa wakikabiliana nao. Amesisitiza kuwa hii leo Israel imeshindwa kukabiliana na vijana wa Kipalestina baada ya mapambano ya Wapalestina kushika sura ya Kiislamu. 363308