Kwa mujibu wa ukurasa wa habari wa Intaneti wa Islamonline, radio ya Kikristo ya FEBC inatangaza aghlabu ya maeneo ya dunia kwa zaidi ya lugha 150. Radio hiyo ina vipindi maalumu vya propaganda za Kikristo zinazolenga kueneza Ukristo katika nchi za Kiislamu na maeneo yenye Waislamu wengi katika nchi mbalimbali duniani.
Lengo kuu la radio ya FEBC (Far East Broadcasting Company) ni kueneza Ukristo katika nchi muhimu za Kiisalmu za Indonesia, Bangladesh, India na Pakistan. Nchi hizo zina zaidi ya nusu ya idadi ya Waislamu wote duniani.
Kazakhstan ambayo imebadilika na kuwa kitovu muhimu cha Uislamu na lango la Asia ya Kati ni kati ya nchi ambazo zinalengwa na Wamishonari wa Kikristo. Mkurugenzi wa FEBC Gregg Harris amenukuliwa akisema: "Sisi tunataka kueneza upendo wa Ukristo miongoni mwa jamii za Waislamu na ili kuwafikia waja wa Mungu tunataka msaada na dua zenu". Amesema, moja ya njia ya kuwavutia Waislamu kuukubali Ukristo ni kuwaambia kuwa Nabii Issa AS ametajwa kwa wema katika Qur'ani Tukufu .
FEBC ni kituo cha radio ya Wakristo cha kimataifa kilichoanzishwa mwaka 1945 baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kwa lengo la kueneza Injili kote duniani. Radio hiyo ina transmita 32 katika maeneo mbalimbali duniani zinazoeneza propaganda za Kikristo hasa miongoni mwa Waislamu. 363873