IQNA

Qur'ani ndio ufumbuzi wa hitilafu za umma wa Kiislamu

16:05 - February 16, 2009
Habari ID: 1744772
Qur'ani Tukufu ndio ufumbuzi wa hitilafu za umma wa Kiislamu na ufunguo wa ufanisi wa mwanadamu. Vilevile Waislamu wote wanaweza kuungana kwa msaada wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa na Pr. Ihsanullah, mhadhiri wa chuo kikuu na mmoja wa wasomi wa Kiislamu wa madhehebu ya Ahlusunna wa Pakistan wakati alipotembelea taasisi ya Darul Hadith mjini Tehran.
Pr. Ihsanullah amesema kuwa kazi kubwa imefanyika katika taasisi hiyo katika medani ya hadithi na kwamba sehemu moja ya kazi hiyo ni uhakiki kuhusu vyanzo vya hadithi za Waislamu wa Kisuni. Vilevile amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na taasisi ya Darul Hadith ya Tehran katika taaluma ya sayansi ya hadithi na akasema kuwa kazi hiyo itawanufaisha watafiti na wahakiki.
Mtafiti huo wa masuala ya Qur'ani amesema kuwa hali ya utafiti wa hadithi nchini Pakistan inaridhisha. Amesema, Waislamu wote duniani hawahitilafiani katika masuala ya Qur'ani na kwamba hitilafu zao zinatokana na hadithi zisizokuwa na itibari.
Wasomi, wanasheria, wawakilishi wa bunge na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Pakistan Jumapili ya jana walitembelea taasisi ya Darul Hadith mjini Tehran. 364641
captcha