IQNA

Kitabu cha "Uislamu na Uhuru" chatarjumiwa na kuchapishwa Italia

11:41 - February 18, 2009
Habari ID: 1745461
Kitabu cha "Uislamu na Uhuru" kilichoandikwa na Ayatullah Muhammad Taqi Misbah Yazdi kimetarjumiwa kwa lugha ya Kitaliano na kuchapishwa na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Italia.
Abbas De Palma ameandika katika utangulizi wa kitabu hicho chenye kurasa 96 kwamba suala la uhuru limezusha mjadala mkubwa katika uhusiano wa Mashariki na Magharibi. Anasema: Uhuru umefasiriwa kimakosa katika ulimwengu wa Magharibi na kupewa maana ya uhuru wa kutenda kila kitu na kutokuwa na mpaka wa aina yoyote. Amesema, Uislamu umeupa uhuru maana chanya na kutambuliwa kuwa ni jambo la kifitra na kimaumbile kwa ajili ya kutakasa moyo na nafsi ya mwanadamu.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Italia amesema kuwa uhuru ni moja ya sehemu muhimu za ujudi na maumbile ya mwanadamu. Amesema kuwa yumkini tukasema kuwa uhuru pamoja na akili ndizo nguzo muhimu za maumbile ya mwanadamu.
Kitabu cha Uislamu na Uhuru kimechapishwa na Taasisi ya Irfan na tayari kimeanza kutolewa kwa wananchi wa Italia. 365338

captcha