Makala hiyo inajadili maudhui ya siku ya waqfu, maana ya waqfu, waqfu zilizotolewa na Mtume (saw) na Ahlubaiti zake (as), mfano wa waqfu zilizotolewa na Imam Ali bin Abi Twalib (as), waqfu katika Qur'ani tukufu na waqfu katika mtazamo wa kihistoria na kifiqhi.
Maudhui nyingine ni nafasi ya waqfu katika kustawisha utamaduni na staarabu wa Kiislamu, mchango wa utamaduni wa waqfu katika maendeleo ya sayansi na elimu, waqfu, nembo ya ustawi wa kibinadamu katika jamii ya kidini, waqfu katika maandiko ya fasihi ya Kifarsi na kadhalika.
Makala hiyo imeeleza kuwa waqfu ni kutenga mali na milki kwa ajili ya kusabilia manufaa yake katika njia za kheri.
Sehemu moja ya makala hiyo imesema: Kwa sasa Waislamu wako katika kipindi cha historia ambako wanalazimika zaidi kutazama upya turathi zao kuliko wakati wowote mwingine. Kwani ustawi na maendeleo ya jamii za Kiislamu hayawezi kupatikana kwa kuiga na kukalidi jamii zisizokuwa za Kiislamu. 367278