IQNA

Mkutano wa wanachuo na maimamu wa swala za jamaa wa Thailand

22:23 - March 03, 2009
Habari ID: 1751328
Wanazuoni wa kidini na maimamu waliohitimu masomo yao katika chuo cha kidini cha mji mtakatifu wa Qum nchini Iran siku ya Ijumaa watakutana katika Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Bangkok.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo hicho, mkutano huo utahudhuriwa na zaidi ya wanazuoni, wanafunzi na maimamu wa kike na kiume waliohitimu masomo yao katika kituo cha kidini cha Qum, ambapo watakutana na kuzungumza na Ayatullah Shahrukhi, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika nchi za Myanmar, Bangladesh na Thailand. Katika kikao hicho, mwanazuoni huyo atazungumzia maisha ya Imam Hassan Askari (as) pamoja na masuala ya maadili.
Vilevile washiriki wa kikao hicho watazungumza na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sheria za Kiislamu. 371491
captcha