Mwendesha baiskeli anayeeneza utamaduni wa Qur'ani Tukufu mkaazi wa Tehran, mji mkuu wa Iran ambaye amebeba ujumbe unaosema, 'Tutafute Njia Sahihi ya Maisha kwenye Qur'ani', amewasili mjini Shiraz baada ya kupita katika mikoa 11.
Mwendesha baiskeli huyo Amir Khodafar aliwasili katika mji huo siku ya Jumatatu alasiri.
Katika safari yake hiyo, Khodafar amepanga kusambaza nyaraka 124,000 kuhusiana na amri za Qur'ani na hadithi za maimamu watoharifu kuhusiana na maisha bora ya Kiislamu, kwa ushirikiano wa Taasisi ya Qur'ani ya mjini Tehran, katika masafa ya karibu kilomita 14,000 kote nchini Iran. 372169